Trofimo wa Efeso (kwa Kigiriki: Τρόφιμος ὁ Ἐφέσιος, Tróphimos ho Ephésios; alifariki Sinnada, Frigia, leo nchini Uturuki[1]) alikuwa Mkristo kutoka mji huo wa Asia Ndogo (Mdo 20:4) aliyeongozana na Mtume Paulo na wenzake wengine katika sehemu ya safari yake ya tatu ya kimisionari hadi Yerusalemu[2].
Kwa kuwa alikuwa mtu wa mataifa (Mdo 21), Wayahudi walidhani kwamba Paulo alimuingiza mpaka ndani kabisa ya Hekalu, sehemu ambayo ilikuwa kwa taifa lao tu (Mdo 21:28). Ndiyo sababu ya jaribio la kumuua Paulo lililoishia katika miaka zaidi ya 4 ya kifungo kati ya Kaisarea Baharini na Roma (58-63).
Baada ya kurudishiwa uhuru, Paulo alimuandikia Timotheo kwamba alimuacha Trofimo huko Mileto kwa sababu ya ugonjwa.[3] Habari hiyo inahusu safari nyingine iliyofuata.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Septemba[4].
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search